Baada ya kuwa na wiki mbaya ya kuwaaga wapendwa wao kwenye klabu yao Sir Alex Ferguson na Paul Scholes, washabiki wa Manchester United wanaweza wakawa wanamkaribisha kipenzi chao Cristiano Ronaldo - ikiwa wao wenyewe wataweza kupata fedha za kumrudisha kutoka Real Madrid.
Kundi la mashabiki wa klabu hiyo kutoka Australia wametengeneza mtandao ambao mashabiki wa United wataweza kuchangia fedha za kuweza kumnunua mchezaji huyo kutoka Real Madrid, Ronaldo ana kiengele ambacho kimemuwekea thamani ya paundi millioni 100 kwa timu yoyote inayomtaka.
Harakati za mtandao wa 'BringRonaldoHome' zimeanza kuzaa matunda baada ya mashabiki maelfu kutuma maombi ya kununua jezi yenye jina la Ronaldo - lakini ili kampeni kufanikiwa inatakiwa wachangiaji millioni 10 watoa kiasi cha £10 kila mmoja ili kutimiza lengo.
Kwa kuwa United wanaripotiwa kuwa na mashabiki mil. 659 duniani kote, kufikisha £100 litakuwa jambo rahisi.
Kampeni hiyo ya kumrudisha Ronaldo OT imezinduliwa siku 3 zilizopita, huku video kibao za mashabiki wa United wakihamasishana zikifurika kwenye mitandao ya facebook na Twitter.
Fedha zitakazopatikana kupitia mtandao huo zitapelekwa kwa United kwa masharti - kuwawezesha kutumia fedha hizo za mchango wa mashabiki kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wa Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid.
Ikiwa United watafanikiwa kumrudisha Ronaldo basi fedha zote zilizopatikana kupitia mtandao huo basi mashabiki wote waliochangia watatumiwa jezi zenye jina la Ronaldo - na ikiwa itashindikana kumrudisha CR7 Old Trafford basi kila aliyechangia atarudishiwa fedha zake.
Mashabiki wanaweza kuchangia kupitia www.bringronaldohome.org/