Sunday, 19 May 2013

JUMLA YA WAREMBO 12 KUWANIA TAJI LA MISS LINDI HAPO MEI 31 MWAKA HUU


Shindano la kumsaka Malkia wa Mkoa wa Lindi ‘Miss Lindi 2013’ linataraji kufanyika Mei 31 mwaka huu katika ukumbi wa Hoteli ya Lindi Beach Resort (Oceanic Hotel).

Akizungumza na Mfuatiliaji wetu mjini Lindi, Mwandaaji wa Shindano hilo, Shaha Ramadhani kupitia kampuni ya Alliance Entertainment amesema warembo 12 wataingia Kambini Hotelini hapo 

Maandalizi yote ya shindano hilo yanaendelea vyema na Milango iko wazi kwa Wadhamini kujitokeza.

Irine Veda (pichani juu) ndiye anashikilia taji hilo baada ya kulitwaa mwaka 2012.