Wednesday, 15 May 2013

HABARI NJEMA KWA WASANII,IKIWA NI JANA TANGU MBUNGE ZITTO KABWE KUTOA PENDEKEZO LAKE BINAFSI KUHUSU KUZUIA UNYONYAJI DHIDI YA WASANII KATIKA BIASHARA YA MIITO

Waziri wa Viwanda na Biashara DR ABDALLAH KIGODA ameagiza mabadiliko ya kanuni katika Sheria ya Hakimiliki ili kuhakikisha kwamba Wasanii wa muziki hapa nchini wanapata mapato stahiki katika biashara ya #RBT . Mirahaba katika biashara ya miito ya simu na matangazo ya televisheni na radio Ni mapato muhimu sana Kwa wasanii. Angalau sasa tunaona Mwanga. Tutaendelea kuishinikiza serikali kulinda wasanii na Hakimiliki zao.