Esma  Abdul ambae ni dada yake mwimbaji staa wa Tanzania, Diamond Platnums,  amesema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya harusi ya Diamond ambae  anatarajiwa kumuoa mtangazaji wa TV aitwae Penny. 
Esma  ambae anaishi nyumba moja na kaka yake amesema, "Tumemkubali sana wifi  yetu na tunampenda kwa sababu mtu yeyote mimi nitakaetambulishwa siwezi  nikamkataa, manake nikimuingilia kwenye mapenzi yake na yeye  ataniingilia kwenye mapenzi yangu." 
Huu  ni mwezi wa tano toka Esma amjue wifi yake ambae ni Penny, anasema  nyumbani amekubalika na mipango ya harusi inaandaliwa japo hajui ni lini  itafanyika, manake hiyo ni siri kwa sasa. 
 Dada yake Diamond aka wifi yake Penny 
Zaidi  ya wiki tano zilizopita, Diamond aliongea na kusema ndoa yake  imekaribia kufungwa na huyo mkewe mtarajiwa ambae ni mjamzito lakini pia  akathibitisha kumnunulia gari la kutembelea aliloliagiza nchini Japan -  Hyundai IX 35. 
Mpaka  sasa Mwimbaji Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa  Tanzania alieandikwa sana kwenye internet 2012, ameshaingia kwenye  headlines za kuwa mapenzini na mastaa wa kike Tanzania kipindi cha nyuma  kama Jokate, Wema Sepetu na wengine.