Tuesday, 14 May 2013

CHELSEA WASAFIRI KUWAFUATA BENFICA, KIPUTE KIZITO KESHO AMSTERDAM ARENA!!

Away we go: The Chelsea team boarded the coach as they started their journey to Amsterdam to take on Benfica in the Europa League final

Wazee wa London, klabu ya Chelsea chini ya kocha wa muda, Mhispania Rafa Benitez wamesafiri kuwafuata Benfica ili kuchuana nao katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Ligi ya Uropa ambapo kipute hicho cha kukata na shoka kitapigwa katika dimba la Amsterdam Arena nchini Uholanzi siku ya kesho.
Asubuhi ya leo Benitez amewasindikiza vijana wake kutoka uwanja wa mazoezi wa Cobham hadi stendi ya basi tayari kwa safari ya kwenda uwanja wa ndege kuelekea Amsterdam.
Benfica  wataingia dimbani kesho huku wakiwa wameshapokwa ubingwa na wapinzani wao wakubwa FC Porto ambao walitwaa ubingwa huo wikiendi iliyopita.
Nahodha wa Chelse John Terry, mshambulizi Eden Harzad na kiungo bora John Obi Mikel nao wamesafiri leo ingawa wapo hatihati kushuka dimbani hapo kesho kutokana na kuwa majeruhi.
Twaenda kuwafuta:  Wachezaji wa Chelsea wakianza safari yao kwenda Amsterdam kuwafuata Benfica katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Ligi ya Uropa.
Frank James Lampard ambaye ndio mchezaji aliyeifungia mabao mengi zaidi Chelsea, kesho anatarajia kuongoza safu ya kiungo akisaidiana na David Luiz pamoja na Ramires ambao watakuwa wanawapelekea mipira Juan Mata na Oscar watakaosimama mbele kutafuta nyavu za Benfica.
Packed up: Juan Mata boarded the coach with a coffee after putting his bags in the hold Juan Mata akiingia na kikombe cha kahawa ili kuburudisha nafsi yake, ama kweli kazi na dawa jamani
Packed up: Juan Mata boarded the coach with a coffee after putting his bags in the hold
Emotional: Chelsea defender David Luiz will return to the club he left for Stamford BridgeDavid Luiz naye amesafiri leo hii kwenda Amsterdam Uholanzi kwa ajili ya kipute cha kesho
Relaxed: Oscar and his Chelsea team-mates look laid back as they make their way to the airport from the Cobham training base Wachezaji wa Chelsea katika basi wakitokeo uwanja wa mazoezi wa Cobham wakielekea uwanja wa ndege