Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wa Pili kutoka kushoto Mbarak Abdulwakil akielekea kwenye lango la kuingia kwenye Ukumbi wa Bunge kuhudhuria kikao cha Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kinachotarajiwa kumalizika leo mjini Dodoma watatu kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mwamini Malemi akifuatiwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Bw. John Minja
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Bw. John Minja wa kwanza kutoka kushoto akifuatiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IJP) Said Mwema, watatu kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Malemi akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mbarak Abdulwakil wa kwanza kulia wakiwa pamoja na watendaji wakuu wengine wa wizara hiyo, wakisikiliza kwa makini hoja zinazotolewa na Wabunge wakati wa kikao cha Bajeti ya wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inayotarajiwa kumalizika leo mjini Dodoma
Sehemu ya watendaji wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pichani wakisikiliza kwa makini hotuba ya bajeti ya wizara yao wakati hotuba hiyo ikisomwa bungeni leo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mbarak Abdulwakil wa kwanza kutoka kulia.
Baadhi ya Makamishna wa Jeshi la Polisi na Magereza wakisikiliza kwa makini hotuba ya bajeti ya wizara yao ya Mambo ya Ndani ya Nchi inayoendelea kusomwa katika Kikao cha Bunge la Bajeti kinachoendelea mjini Dodoma leo, Bajeti ya Wizara hiyo inatarajiwa kukamilika leo.
Baadhi ya Maafisa Bajeti wa Idara ya Uhamiaji wakiandaa majibu kwa ajili ya kujibu hoja mbalimbali zinazotolewa na Waheshimiwa Wabunge katika kikao cha Bunge la Bajeti kinachojadili hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyoanza kusikilizwa jana mjini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi wasaidizi , Makaimu Kamanda na Maafisa wa Bajeti wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiandaa majibu kwa ajili ya kujibu hoja za Wabunge katika kikao cha Mawasilisho ya hotuba ya Bajeti ya wizara hiyo kinachotarajiwa kukamilika leo mjini Dodoma.
Picha na:Christina Mwangosi
Afisa Habari
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi