Wednesday, 8 May 2013

BREAKING NEWS: SIR ALEX FERGUSON ATANGAZA KUSTAAFU KUIFUNDISHA MANCHESTER UNITED - KUWA BALOZI NA MKURUGENZI SASA

 
Sir Alex Ferguson ametangaza kustaafu kuifundisha Manchester United baada ya miaka 27 ndani ya Old Trafford.
Taarifa za Fergie kutaka kustaafu zilianza kuzagaa tangu jana mchana na usiku zikazidi lakini hakuna habari yoyote rasmi iliyotoka United mpaka leo asubuhi.
 
Ferguson aliwasili kazini kama kawaida asubuhi akiendesha gari lake katika uwanja wa mazoezi wa United wa Carrington mnamo saa kumi na mbili.

Akitangaza uamuzi wake wa kustaafu alisema: "Uamuzi huu nimeufikiria sana na sikukurupuka. Ni muda sahihi.
 
'Ilikuwa ni muhimu kuiacha taasisi hii ikiwa katika hali nzuri na imara na ninaamini nimefanya kazi nzuri sana. Ubora wa kikosi hiki kilichoshinda ligi, na uwiano wa umri wa wachezaji unaonyesha kutaendelea kuwepo na mafanikio katika hatua ya juu - mfumo mzuri wa kukuza vipaji unatoa picha nzuri ya mafanikio ya siku zijazo ya klabu.

'Kutokea hapa, nina furaha kuchukua majukumu ya ukurugenzi na ubalozi wa klabu hii. Sasa naangalia mbele kuzitendea haki kazi zangu.

'Lazima niipe shukrani familia yangu, mapenzi yao na sapoti imekuwa muhimu sana kwangu. Mke wangu Cathy amekuwa mtu muhimu katika maisha yangu yote, kunipa moyo pale mambo yalipokuwa hayaendi sawa na kunisapoti. Maneno hayatoshi kuelezea namna gani wakati huu ulivyo kwangu.

'Kwa wachezaji wangu na wafanyakazi wengine wa klabu, wa sasa na zamani, ningependa kuwashukuru kwa kazi nzuri tuliyofanya pamoja iliyonisaidia kuleta kumbukumbu nyingi za ushindi zisizosahaulika. Bila mchango wao historia ya klabu hii kubwa isingekuwa tajiri kiasi hiki.

'Katika miaka yangu ya mwanzo hapa, utetezi wa bodi kwangu, na Sir Bobby Charlton zaidi, ulinipa hali ya kujiamini na muda wa kujenga timu ya soka.

'Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, familia ya Glazer imenipa kila kitu nilichohitaji katika kuiongoza Manchester United kwa ubora wote na nimekuwa nina bahati sana kuweza kufanya kazi na mtu mwenye kipaji na mwaminifu kama CEO David Gill, Nina washukuru sana.

'Kwa mashabiki, shukrani sana. Mapenzi na sapoti mliyonipa miaka yote siwezi kuielezea. Imekuwa ni heshima kubwa sana kuweza kuiongoza klabu yenu na nimekuwa na ufahari wa muda wangu kama kocha wa Manchester United." alimaliza Ferguson.

HAYA NDIO MAFANIKIO YA FERGUSON KAMA KOCHA
ST MIRREN
Scottish First Division (1): 1976-77.

ABERDEEN
Scottish Premier Division (3): 1979-80, 1983-84, 1984-85.
Scottish Cup (4): 1981-82, 1982-83, 1983-84, 1985-86.
Scottish League Cup (1): 1985-86.
European Cup Winners' Cup (1): 1982-83.
European Super Cup (1): 1983.

MANCHESTER UNITED
Premier League (13): 1992-93, 1993-94, 1995-96, 1996-97, 1998-99, 1999-2000, 2000-01, 2002-03, 2006-07, 2007-08, 2008-09, 2010-11, 2012-13.

FA Cup (5): 1989-90, 1993-94, 1995-96, 1998-99, 2003-04.
League Cup (4): 1991-92, 2005-06, 2008-09, 2009-10.

Charity/Community Shield (10): 1990 (shared), 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011.
Champions League (2): 1998-99, 2007-08.
European Cup Winners' Cup (1): 1990-91.
European Super Cup (1): 1991.
Intercontinental Cup (1): 1999.
FIFA Club World Cup (1): 2008.