KOCHA wa Chelsea, Rafael Benitez ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi April Ligi Kuu England baada ya kuiongoza timu yake kucheza mechi nne bila kufungwa, wakati mshambuliaji wa Manchester United, Robin van Persie ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora.
Mafanikio haya yanakuja saa kadhaa baada ya kocha wa Manchester United, Alex Ferguson kusema Benitez ndiye mtu pekee anayemvutia akiwa kazini Stamford Bridge.
Robin van Persie ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kwa mara ya pili msimu huu, baada ya kushinda pia na mwezi Desemba.
Mjuzi: Rafael Benitez amechaguliwa kocha bora wa April Ligi Kuu England
Mkali wa wakali: Robin van Persie ameshinda tuzo ya tano ya Mchezaji Bora wa Mwezi
TUZO ZA BENITEZ KOCHA BORA MWEZI
Novemba 2005 - Liverpool
Desemba 2005 - Liverpool
Januari 2007 - Liverpool
Oktoba 2008 - Liverpool
Machi 2009 - Liverpool
Aprili 2013 - Chelsea
Mara ya mwisho kocha wa Chelsea kushinda tuzo hiyo ilikuwa ni Aprili mwaka 2011, ilipochukuliwa na Carlo Ancelotti kabla hajatupiwa virago na klabu.
Pamoja na kukandiwa sana na mashabiki wa Chelsea, Benitez ameendelea kufanya vizuri sasa akiwania nafasi ya tatu katika Ligi Kuu na tayari ameiwezesha timu kutinga fainali ya Europa League kwa kishindo.
WACHEZAJI BORA WA MWEZI 2012/2013
Steven Fletcher (Sunderland) - Septemba
Juan Mata (Chelsea) - Oktoba
Marouane Fellaini (Everton) - Novemba
Robin van Persie (Man United) - Desemba
Adam le Fonde (Reading) - Januari
Gareth Bale (Tottenham) - Februari
Jan Vertonghen (Tottenham) - Machi
Robin van Persie (Man United) - Aprili
Muuwaji: Van Persie bao lake la mwisho alifunga kwa penalti dhidi ya klabu yake ya zamani, Arsenal
MAKOCHA BORA WA MWEZI 2012/2013
David Moyes (Everton) - Septemba 2012
Alex Ferguson (Man United) - Oktoba 2012
Steve Clarke (West Brom) - Novemba 2012
Andre Villas-Boas (Tottenham) - Desemba 2012
Brian McDermott (Reading) - Januari 2013
Andrew Villas-Boas (Tottenham) - Februari 2013
David Moyes (Everton) - Machi 2013
Rafael Benitez (Liverpool) - Aprili 2013