Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alphonso Lenhardt akikata utepe kuashiria kuzindua jengo la maabara ya kisasa ya magonjwa mbalimbali katika hospitali ya rufaa Mbeya |
Hapa barozi akizindua maabara ya kisasa ya ugonjwa TB |
Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alphonso Lenhardt akizungumza na watumishi wa afya kabla ya kuzindua maabara ya kisasa ya kimataifa ya magonjwa mbalimbali |
Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dk. Eliuter Samky aliwashukuru watu wa Marekani kwa kuendelea kutoa misaada katika Mkoa wa Mbeya hususani sekta ya Afya. |
Baadhi ya watumishi wakimsikiliza barozi wa Marekani |
Moja ya wataalamu wa idara ya kifua kikuu akimweleza barozi jinsi vipimo mbali mbali vya TB vinavyopimwa katika maabara hiyo aliyoizindua barozi huyo |
Barozi akiangalia mashine ya kutotolea vifaranga alipotembelea kituo cha shdepha |
Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alphonso Lenhardt aliwashukuru watanzania kwa kuendelea kushirikiana naye na kuwaahidi kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Shdepha Tanzania hususani Mkoa wa Mbeya. |
Mkuu wa Kituo cha Afya na Maendeleo kwa ajili ya Watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(SHDEPHA) Mkoa wa Mbeya Olivia Mahenge wakati akimkaribisha Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alphonso Lenhardt alipotembelea kituo hicho kilichopo Sae Jijini Mbeya. |
Barozi akipokea zawadi toka kwa Olivia Mahenge |
WATANZANIA wametakiwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mashirika ya nchi za nje namna wanavyopambana kuzuia na kupunguza maambukizi virusi vya Ukimwi kwa nchi za Afrika hususani Tanzania. Mwito huo ulitolewa na Mkuu wa Kituo cha Afya na Maendeleo kwa ajili ya Watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(SHDEPHA) Mkoa wa Mbeya Olivia Mahenge wakati akimkaribisha Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alphonso Lenhardt alipotembelea kituo hicho kilichopo Sae Jijini Mbeya. Alisema Watanzania wako mstari wa nyuma katika kuiga juhudi zinazofanywa na watu kutoka nchi za Ulaya namna wanavyopambana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Maleria kwa vitendo. Katika risala yao kwa Balozi huyo walisema Shdepha Mkoa wa Mbeya imepata mafanikio makubwa kutoka Msaada wa Watu wa Marekani ambapo Balozi ameshatembelea kituo hicho kwa mara ya pili ambapo mara ya kwanza alitembelea Mwaka 2009. Walisema mbali na kutoa huduma na ushauri kwa waathirika juu ya kujikinga na maambukizi mapya pia hufanya shughuli ndogo ndogo kama ufugaji, kilimo na Ujasiliamali ambapo hutengeneza Sabani na Chaki pamoja na Vitambaa. Hata hivyo walisema kuna changamoto ambazo zinawakabili kama ukosefu wa Fedha za kuwekea umeme mkubwa kwa ajili ya vifaa vya kutengenezea sabuni kutokana na umeme uliopo sasa kuwa mdogo ambapo walisema wanahitaji zaidi ya Milioni 6. Waliongeza kuwa katika kituo hicho kina jumla ya watumishi ambao zaidi ya Asilimia 70 wanaishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi hivyo wanaulewa mkubwa kuhusu madhara hayo ili kuwashauri wenye matatizo na wenye mambukizi. Kwa upande wake Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alphonso Lenhardt aliwashukuru watanzania kwa kuendelea kushirikiana naye na kuwaahidi kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Shdepha Tanzania hususani Mkoa wa Mbeya. Alisema kwa niaba ya Watu wa Marekani wataendelea kutoa msaada kwa Mkoa wa Mbeya kuhusu mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi tokea waanze kwa Miaka Nane iliyopita na kwamba kwa sasa Programu 150 zinazohusu afya ni zaidi ya 40 zilizopo Nyanda za Juu kusini. Aidha Balozihuyo yupo Mkoani Mbeya kwa Ziara ya Siku mbili ambapo katika siku ya kwanza Balozi huyo alizindua Maabara ya Kisasa ya Kimataifa ya Magonjwa mbali mbali katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya. Maabara hiyo ambayo itajikita katika ugonjwa wa Kifua kikuu imepewa kibali na Cheti kutoka Umoja wa Mataifa ambayo itakuwa maabara ya pili kufunguliwa Mkoani Mbeya baada ya kuwepo Hospitali ya Mhimbili Dar Es Salaam. Balozi huyo alidai kwamba katika makubaliano ya Ushirikiano kati yaSerikali ya Watu wa Marekani na Tanzania ya kusaidiana na kudumisha undugu ni lazima yatekelezwe kwa vitendo kutokana na kuthamini afya za watanzania. Alisema tangu Mwaka 2008 Serikali ya Marekani imekuwa ikishirikiana na kukubaliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Tanzania kuhakikisha inatoa msaada wa kiafya kwa Watanzania kupitia Mpango wa dharula wa Raisi wa kupunguza makali ya Ukimwi uliofadhiliwa na Watu wa Marekani. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dk. Eliuter Samky aliwashukuru watu wa Marekani kwa kuendelea kutoa misaada katika Mkoa wa Mbeya hususani sekta ya Afya. Picha na Mbeya yetu |