MTALIANO Mario Balotelli amefunga mabao  mawili usiku huu ikiwemo penalti babu kubwa, akiiwezesha AC Milan kupata  nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuichapa Pescara  mabao 4-0.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester  City alifunga bao lake la kwanza kwa penalti kabla ya kufunga lingine  katika mechi ambayo wachezaji wengine waliowahi kucheza Ligi Kuu ya  England Sulley Muntari na Mathieu Flamini walifunga.
Amekuwa na mafanikio tangu arejee Italia  na Milan wamekuwa hawafungwi katika mechi ambazo anacheza Serie A,  ikishinda nane na kutoa sare tatu. 

Mario Balotelli akifunga kwa mkwaju wa penalti

Balotelli akishangilia na Robinho

Waliocheza England wanatisha: Sulley Muntari akishangilia bao lake

Balotelli akimtoka Marco Capuano 

Wachezaji wa Milan wakishangilia