MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo amejikuta katikati ya mvuatno wa klabu mbili kuwania saini yake,Manchester United na Chelsea.
Nyota huyo mwenye thamani ya Pauni Milioni 80 wa Real Madridd, ambaye alipewa kadi nyekundu jana katika fainali ya Copa del Rey waliyofungwa na Atletico, yumo kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa na kocha mtarajiwa wa Chelsea, Jose Mourinho.
'The Special One' pia alipandishwa jukwaani baada ya kubishana na refa jana katika mechi mbaya upande wao Uwanja wa Bernabeu jana.
United watakuwa na nafasi ya kwanza ya kumsajili Ronaldo ikiwa Real wataamua kumuuza hivyo Mreno huyo ana nafasi kubwa ya kurejea Old Trafford.
Lakini Mourinho, ambaye amekuwa akifanya naye kazi kwa miaka mitatu iliyopita, amemuweka katika orodha wake ya nyota anaowahitaji mno.
Anatakiwa: Mourinho anatumai kuondoka na Ronaldo kutoka Real Madrid kwenda Chelsea
Wayne Rooney, ambaye angependa kwenda Chelsea, na mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani pia anatakiwa na Mourinho.
Ronaldo amecheza misimu minne Real Madrid, lakini amejikuta anachanganyikiwa kutokana na kutoheshimika katika klabu hiyo.
Mmoja wa bora: Ronaldo amefunga bao lake la 55 msimu huu Real Madrid usiku wa jana
Chelsea haijazungumzia lolote juu ya hayo, lakini Roman Abramovich anajiandaa kutumia fedha nyingi kipindi hiki cha usajili.
Kocha wa Muda wa Chelsea, Rafa Benitez amesema jana kwamba Abramovich atatoa Pauni Milioni 100 za usajili kwa kocha mpya.
Wamo kwenye orodha: Wayne Rooney wa Manchester United (kushoto) na Edinson Cavani wa Napoli (kulia) pia wanatakiwa na Mourinho
Fungu la usajili: Abramovich atampa Mourinho Pauni Milioni 100 za usajili