Mpira umetinga nyavuni, ni bao la kwanza katika mchezo wa leo Uwanja wa Prince Moulay Abdellah lililofungwa na John Bocco 'Adebayor' wa Azam FC kwa mpira wa adhabu. Katika mchezo huo wa marudiano, Raundi ya Tatu Kombe la Shirikisho Afrika, wenyeji AS FAR Rabat walishinda 2-1 na kusonga mbele. |
Kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy' akiwatoka wachezaji wa AS FAR Rabat |
Kipre Tchetche wa Azam akimtoka beki wa AS FAR Rabat |
Khamis Mcha 'Vialli' akimtoka beki wa AS FAR Rabat |
Brian Umony akimtoka beki wa AS FAR Rabat |
Humphrey Mieno wa Azam kushoto akigombea mpira wa juu na kiungo wa AS FAR Rabat |
Kipre Tchetche na kipa wa Azam |
Polisi wakipambana na mashabiki wa AS FAR Rabat |
Sure Boy akituliza mpira gambani ... |
Mashabiki wa AS FAR Rabat wakimsaidia mwenzao aliyeumia katika mapambano na Polisi |
Polisi na mashabiki wa AS FAR Rabat... |
Kipa wa AS FAR Rabat akiuwahi mpira |
Azam wakishangilia bao lao |
Kipre Tchetche kulia akiwania mpira |
Haikuwa bahati yao; John Bocco akishangilia bao lake, anayemfuata ni Kipre Tchetche |
David Mwantika akimkwatua mchezaji wa AS FAR Rabat |
Maseneta wa Azam FC... |
Beki wa Azam FC, Mkenya Joackins Atudo akimdhibiti mshambuliaji wa AS FAR Rabat |
Waziri Salum akitafuta mbonu za kumpokonya mpira mchezaji wa AS FAR Rabat |
Kikosi cha AS FAr Rabat leo |
Kikosi cha Azam leo |
Beki wa Rabat akiondosha mpira hatarini mbele ya Kipre Tchetche |
Kipa wa AS FAR Rabat amedaka |
Kipre Tchetche anafumua shuti |
Kipre Tchetche akipambana... |
Khamis Mcha 'Vialli' akikabiliana na beki wa AS FAR Rabat |