Khamis Mcha 'Vialli' wa Azam anawania tuzo ya Mwanasoka Bora Tanzania
AZAM FC imeingiza wachezaji wawili katika kinyang’anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora kwenye Tuzo za Wanamichezo Bora Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) 2012/2013 ambao ni Khamis Mcha ‘Vialli’ na John Bocco ‘Adebayor’.
Katika kipengele hicho, nyota hao wawili wa Azam watachuana na Kevin Yonda wa Yanga, Shomary Kapombe wa Simba anayeshikilia tuzo hiyo, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, wote wa TP Mazembe ya DRC.
Azam imeingia mchezaji mmoja katika kipengele cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kigeni anayecheza Tanzania, ambaye ni Kipere Herman Tchetche kutoka Ivory Coast atakayechuana na Mganda Emmanuel Okwi aliyekuwa Simba kwa sasa ameuzwa Etoile du Sahel ya Tunisia.
Katika kipengele hiki, Yanga SC imeingiza wachezaji wawili ambao ni Haruna Niyonzima kutoka Rwanda na Hamisi Kiiza kutoka Uganda.
Upande wa wanasoka wa kike, Fatuma Mustafa atachuana na Asha Rashid, Mwanahamisi Omary, Sofia Mwasikili anayeshikilia tuzo huyo na Esther Chabruma.
Katika mpira wa magongo wanaume Sylvester Kigodi atachuana na Castor Mayuma, Gurtej Bilu Singh, Vendri Bhamra na Elias Samala. Gofu ya Kulipwa; Hassani Kadio, Yassin Salehe, Fadhili Nkya, Salimu Mwanyenza na Rajabu Iddy.
Gofu Ridhaa wanawake; Madina Iddi, Angel Eaton, Hawa Wanyeche, Ayne Magombe na gofu ya Ridhaa wanaume, Jimmy Mollel, Frank Roman, Nuru Mollel, Martin MacDonald na John Said.
Katika ngumi za Ridhaa wanaume; Ismail Isack Galiatano, Said Hofu, Selemani Kidunda, Victor Njaiti na Mohamed Chibumbui na kwa wanawake, Sara Andrew, Irene Kimaro, Easther Kimbe, Mather George na Mariam Nyerere.
Ngumi za Kulipwa; Francis Miyeyusho, Ramadhan Shauri, Thomas Mashali, Said Mbelwa na Francis Cheka. Judo Bara Wanaume; Ahmed Magogo, Andrew Mlugu, Geoffrey Mtawa, Gervas Chilipweli, Abuu Mcheteko na Abubakar Nzige. Judo Wanawake Bara; Matrida Temba, Amina Mohamed.
Judo Zanzibar Wanaume; Mohamed Khamis Juma, Masoud Amour Kombo na Mbarouk Suleiman wakati kwa wanawake visiwani humo ni Grace Alphonce na Laylati Mohamed.
Katika Tenisi wanawake ni Rehema Athumani, Vailety Peter, Mkunde iddi, Edna John na Zuhura Baraka wakati kwa Wanaume ni Omary Abdallah, Yassin Shaaban, Hassan Kassim, Kiango Kipingu na Lebric Jacob.
Mpira wa Mikono Wanaume; Faraji Shaibu, Hemedi Salehe, Abinery Kusena, Ally Khamis na Hassan Yussuf wakati kwa wanawake ni Catherine Mapua, Dorris Mangara, Zakia Mohamed, Happy Mahinya na Mary Kimiti.