The Gunners wamemtambulisha Mpoland huyo kama mrithi wa Bacary Sagna kama hawataweza kutatua suala la mkataba wa Mfaransa huyo.
Beki wa kulia wa Feyenoord, Daryl Janmaat pia ametambulishwa kama mmoja wa watu wanaowaniwa.
Atatua Emirates? Beki wa kulia wa Borussia Dortmund, Lukasz Piszczek (kushoto) anaweza kuhamia Arsenal
Piszczek amekuwa akiichezea Dortmund tangu mwaka 2010 aliposajiliwa kama mchezaji huru kutoka Hertha Berlin.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa mmoja wa mabeki wa kulia tishio duniani akitamba katika Bundesliga na timu yake ya taifa, Poland.
Baada ya kufanya vizuri katika michuano ya Euro 2012 ambayo wenyeji hawakufurukuta, Piszczek alianza kumulikwa na Chelsea akawe mbadal wa Jose Bosingwa.
Mustakabali wa Sagna bado upo kizani na Gunners baada ya mazungumzo kuhusu mkataba mpya kuvunjika mwesi uliopita baada ya kuomba ahamie PSG.
Mfaransa huyo amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa.
The Gunners wako hatarini kumpoteza Bacary Sagna (kushoto)