Monday, 13 May 2013

AFANDE SELE AMSHUKURU MH. ZITTO KABWE KWA KUGHARAMIA VIDEO YAKE, HIKI NDO ALICHOKISEMA

 
 
Mapema asubuhi hii Mfalme wa Rhymes Afande Sele ametoa ya moyoni na kuelezea lengo lake la kutunga wimbo wa DINI TUMELETEWA kumrudisha Muafrika kwenye Uafrika na msingi wake wa UMOJA, USHIRIKIANO na UPENDO.

Pia hakuwa nyuma kutoa shukrani zake kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe kwa kumuwezesha kugharamia Video ya wimbo wake huo mpya ambao unafanya vizuri sana kwa sasa.

Nanukuu "Lengo la hii kazi yangu mpya DINI TUMELETEWA ni kumrudisha mwafrika kwenye uafrika wake ambao msingi wake ni UMOJA, USHIRIKIANO NA UPENDO. Ambao kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia ukitoweka. Tumeona mapigano/mauaji ya itikadi za kidini wenyewe kwa wenyewe, pia kuelezea uhuru wa kuabudu kwa imani yoyote bila kuvunja sheria za Taifa letu. Kwa mtu yoyote makini mwenye mapenzi mema kwa Taifa letu na AFRIKA hawezi kupingana na hilo, kwa kutambua hilo MH; 

ZITTO ZUBERI KABWE(ZZK) kajitolea kugharamia gharama zote kwa ajili ya kufanikisha video bora kabisa ya wimbo huu, hii ni kazi yetu wote mimi na wewe, tunasema asante sana kwa Mh; Zitto. AMANI NA UPENDO KWANZA"