Monday, 29 April 2013

WAZIRI MEMBE ASEMA YEYE SIO FISADI NA HANA TUHUMA ZA RUSHWA MWENYE SKENDO YAKE AJITOKEZE HADHARANI

 

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe ataka  kiongozi ama mtu yeyote anayeweza  kutoa  tuhuma  zake dhidi ya Rushwa  kujitokeza hadharani na kumtaja .

Waziri  Membe  alitoa kauli  hiyo leo   katika  ukumbi  wa  ST. Dominic mjini Iringa  wakati akizungumza na  wanavyuo  vya  mkoa  wa  Iringa katika  kongamano  la vyuo vya elimu ya juu mkoani Iringa.

Alisema  kuwa yeye ni miongoni  mwa  viongozi  safi na hajapata  kutoa wala  kupokea rushwa  kwani ana uzalendo mkubwa kwa Taifa  lake  la Tanzania.


 Hata  hivyo amewataka  wasomi wa  vyuo  vikuu  mkoani Iringa  kuongeza  jitihada katika elimu  ili  kuweza  kuja  kuwa  viongozi  wazuri na kuwa  ni vigumu  kuwa  kiongozi mzuri  bila elimu.

Alisema  kuwa  ili  kuwa na  serikali  bora  ni vema  suala la elimu  likapewa  kipaumbele na  wasomi wa  vyuo  vikuu  kuongeza  jitihada zaidi katika  elimu  ili hata  pale  wanaposimama kugombea nafasi  za uongozi ni lazima  wawe  wenyewe  kuwa na uelewa mpana  ili kiongozi bora  atakaye  simamia miji

Kwani  alisema  kuwa  hivi  sasa  kuna ushindani mkubwa wa elimu katika ulimwengu na kama wanafunzi  wataendelea  kufanya mchezo katika  elimu  upo  uwezekano mkubwa wa kuendelea  kushindwa katika soko la ajira.

Hata  hivyo  alisema  kuwa suala la  uzalendo  linahitajika  zaidi kwa  viongozi  ili  kulifanya Taifa  la Tanzania  kuendelea  kuheshimika  ndani na nje ya nchi  ya  Tanzania .

" Mimi   kuna  wakati mmoja mwaka  2005  nikiwa mbunge  nilipata  kuchukua usafiri  wa Taxi ya  kukodi kutoka uwanja  wa Ndege  wa  mwalimu Nyerere  hadi nyumbani  kwangu na nikiwa njiani  dereva wa  taxi  niliyokodi  alianza  kueleza ubaya  wa Tanzania  toka mwanzo hadi mwisho na nilipofika karibu na nyumbani  nilimsimamisha na kumwambia kuwa  sitakulipa pesa yako .....kweli  watanzania  tumekuwa ni  watu  wa kuelezea ubaya  wa Taifa  bila kuangalia  tunazungumza na nani"

Aidha alipingana na  watu ambao  wamekuwa  wakizitolea  nchi ndogo na kuilinganisha na  Tanzania ambalo ni Taifa  kubwa  ukilinganisha na baadhi ya nchi barani Afrika ambazo ni ndogo zaidi

Kuhusu  suala la rushwa  waziri Membe  alisema kuwa  kiongozi  bora  ni yule ambae anachukia  rushwa kwa  vitendo na kujali zaidi  maslahi ya Taifa  badala ya  kuangalia maslahi  binafsi .

Bila  kumtaja  kiongozi  yeyote  ama mtu  yeyote  waziri Membe  alisema  kuwa ni lazima  suala la Rushwa  kukemewa na kila mmoja  wetu na kuwa  ni vigumu  kuwa  kiongozi bora kama utakuwa  ukipokea Rushwa.

Kwa  upande  wake mchokoza mada katika  kongamano  hilo
Dr. Bukaza Chachage alimpongeza  waziri Membe  kwa kauli yake  ya  kuwataka  wale  wote  wanaweza kumtuhumu  kupokea  Rushwa  kupita  mbele na kusema hadharani .