Sunday, 28 April 2013

WACHEZAJI WOTE WA MANCHESTER UNITED SASA KUVAA MEDALI ZA UBINGWA BAADA YA SHERIA MPYA KUPITISHWA


Wachezaji wote wa mabingwa  wapya wa ligi kuu ya England watapata medali za ubingwa wa ligi kuu ya England baada ya chama cha soka che England na ligi kuu kulegeza masharti yaliyokuwa yanabana idadi ya wachezaji wanaoweza kupewa medali pale timu inapotwaa ubingwa.

Katika misimu ya miaka ya nyuma wachezaji waliokuwa wanaweza kupewa medali baada ya timu kuwa bingwa ni wale waliocheza idadi ya mechi 10 na zaidi huku magolikipa pekee wakiwa na nafasi ya upendeleo, zaidi ya hapo kama idadi ya medali ni ndogo timu ilikuwa inatakiwa kutuma maombi maalum ambayo yalihitaji kuridhiwa na FA kuhusu medali za ziada.

Hata hivyo kwa sheria mpya ya ligi kuu ya England, wachezaji wanaoweza kuvaa medali ni wale waliocheza mechi tano na zaidi huku timu inayotwaa ubingwa ikipewa medali 40 na kutakiwa kutuma maombi kwa wale wanaoweza kuwa wamekosa medali hizo.

Kwa sheria za zamani wachezaji Darren Fletcher, Alexander Buttner  na Nick Powell wasingeweza kupewa medali huku kipa Anders Lindergaard akipata kwa sababu sheria hiyo ilikuwa haiwahusu makipa, hata hivyo kwa sasa wachezaji hawa watapata medali kama kawaida huku kukiwa na nyongeza ya kutosha kuwapa wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza ambao hawapati nafasi za kucheza kama Ben Amos, Jesse Lingard na Marnick Vermijl na mchezaji Adnani Januzaj ambaye anacheza kwenye kikosi cha U-18 ambaye amepewa jezi namba 44 huku kocha Sir Alex Fergusson akiahidi kumpa nafasi kwenye mechi zilizobaki.

Fergie ameipa dole sheria hiyo akisema kuwa iko ‘fair’ kwa kuwa kila mchezaji hata kama amecheza mechi tatu kama kina Powell, Fletcher na Buttner anahesabika kuwa ametoa mchango unaostahili medali.