Sunday, 28 April 2013

TASWIRA YA BENKI YA CRDB KATIKA KUKABIDHI WODI HOSPITALI YA RUFAA MOROGORO.

Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii, Daktari Seif Rashid akipaka rangi ukuta wa wodi ya watoto hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya benki CRDB kufanya ukarabati na kughalimu kiasi cha fedha sh50 Milioni mkoani Morogoro. kulia ni Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo.  

Hapa Mkurugenzi mkuu wa benki ya CRDB Dr Charles Kimei akijiandaa kupaka rangi na Naibu waziri Dr Seif Rashid kabla ya kupanda miti na kuzindua rasmi wodi hiyo. 
 

Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Dr Godfrey Mtei naye akishiriki katika zoezi hilo. 
 
Fundi akiendelea na kazi ya kupaka rangi.

ZOEZI LA UPANDAJI WA MITI NDANI YA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA MOROGORO.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakiwa wamebeba miche za miti tayari kwa zoezi la kuanza kupanda miti hiyo ambapo viongozi mbalimbali walipata kila mmoja wao kama kumbukumbu na utunzaji wa mazingira.
 
Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii, Dr Seif Rashid akipanda mti kabla ya viongozi wengine kufanya tukio hilo
 
Mkurugenzi mkuu wa benki ya CRDB Dr Charles Kimei naye akipanda mti wake. 
 
 
Mohamed Hood ambaye ni mmiliki wa basi ya Hood transipot LTD kushoto akipanda mti katika zoezi hilo. 
 
 
Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Dr Godfrey Mtei kushoto akipanda mti.
 
 
 
Mmoja wa maafisa wa benki ya CRDB naye akishiriki kupanda mti
 
  
Mwandishi wa chanel Ten Morogoro Jimmy Mengele akichukua picha kwa MC kwa ajili ya habari katika kituo hicho.
 
Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii, Daktari Seif Rashid wa kwanza kulia akimsikiliza  Mohamed Hood ambaye ni mmiliki wa mabasi ya Hood transipot LTD mara baada ya kumalizika kwa shughulizi za uzinduzi wa wodi hiyo, kushoto ni Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Dr Godfrey Mtei na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Steven Mashishanga.
 
 
Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakitoa burudani kwa kucheza muziki baada ya kumalizika kwa shughulizi za uzinduzi wa wodi hiyo.