polisi Iringa wakiwa katika eneo la Mashine tatu, kuondoa mawe na magogo ambayo yalitumika kuziba barabara hiyo kama sehemu ya kushinikiza serikali kuwaruhusu kuendelea kufanya kazi ya umachinga eneo hilo lisiloruhusiwa
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ikiwa imekutana mchana huu kwa kikao cha dharula kufuatia Machinga kutekeleza kauli ya mbunge Msigwa ya kuvunja sheria |
Hii ndio hali halisi iliyopo eneo la mashine tatu baada ya machinga kurejea eneo hilo leo Hatua hiyo ya machinga kurejea katika eneo hilo la barabara imeonyesha kuichanganya serikali ya mkoa wa Iringa na kulazimika kukutana kwa masaa kadhaa na kamati ya ulinzi na usalama. Akizungumzia suala hilo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa na kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Leticia Warioba ambae ni mkuu wa wilaya ya Iringa alisema kuwa serikali ya mkoa inapinga kwa nguvu zote kitendo cha wafanyabiashara hao kurejea eneo hilo. Dr Warioba alisema kuwa anashangazwa na hatua ya mbunge Msigwa kuwaruhusu wafanyabiashara hao kuvunja sheria wakati mbunge huyo katika vikao vya baraza la madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni diwani ni katika maamuzi ya kuwatoa wafanyabiashara hao alishiriki . Hata hivyo Dr Warioba aliwataka wafanyabiashara hao kwa jumapili ijayo kutofanyabiashara eneo hilo na kuonya wale wote watakaokiuka kauli hiyo na sheria iliyowekwa juu ya kutofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi. Kwa upande wake mwanasheria wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Innocent Kihaga alisema kuwa eneo hilo kisheria limepigwa marufuku kwa biashara za umachinga na kuwa kwa mtu ambae atapatikana akifanya biashara hapo faini yake ni shilingi 50,000 ama kifungo cha miezi sita jela ama vyote kwa pamoja. Wakati huo mbunge wa jimbo la Mbeya mjini ,Joseph Mbilinyi (MR SUGU) leo ameonekana katika Manispaa ya Iringa akiingia katika mashine ya kutoa pesa ATM ya NMB iliyopo nje ya jengo hilo la Manispaa ya Iringa na kusalimiana na viongozi wa Manispaa waliokuwepo nje ya jengo hilo. credit mzee wa matukio daima |