 
 Namba  huwa hazidanganyi. Mabao mawili ya Cristiano Ronaldo katika ushindi wa  mabao 3-0 dhidi ya Athetic Bilbao jana jumapili yalimfanya mreno huyo  kutimiza mabao 50 ndani ya msimu wa 2012-13, akifuata nyayo za mpinzani  wake Lionel Messi ambaye tyari ameshatimiza idadi hiyo ndani ya msimu  huu. Wachezaji hao wawili ndio wachezaji pekee kuweza kufika mabao zaidi  ya 50 ndani ya msimu mmoja katika soka la nchi la Hispania - na  wameweza kufanya hivyo ndani ya misimu mitatu mfululizo.
Messi  hakuwepo kwenye mechi ya ushindi wa Barcelona dhidi ya  Zaragoza 3-0  pale La Romareda. Muargentina huyo amepewa mapumziko ili awee kuwa fiti  zaidi kutokana na majeruhi ya nyama za paja aliyoyapata kwenye mchezo wa  kwanza wa robo fainali ya Champions League dhidi ya Paris  Saint-Germain.
Lakini  nahodha huyo wa Argentina tayari ameshafunga mabao 57 ndani ya msimu  huukatika michezo 46 aliyoichezea Barcelona, na Ronaldo ameifikia rekodi  ya mabao 50 jana usiku. 
MESSI & RONALDO: THE 50-GOAL SEASONS

season
2010-11
2011-12
2012-13 
Messi
53 goals
73 goals
57 goals 
Ronaldo
53 goals
60 goals
50 goals
Ronaldo  alifungua kitabu cha mabao kwa goli lake la haraka zaidi kwenye maisha  yake ya soka, goli la faulo katika sekunde ya 71 ya mchezo, akishindwa  kufikia rekodi ya goli la haraka zaidi la Xerez aliyefunga sekunde ya 45  mwaka 2009.
Kabla  ya baadae hajawakatisha tamaa Athletic ambao walikuwa wanakuja juu  kutafuta goli kwa goli la kichwa na hivyo kufikisha mabao 50 ndani ya  msimu katika mechi 48.
Messi  na Ronaldo walimaliza msimu wa 2011-12 wote wakiwa na mabao 53 (Leo  katika mechi 55; Cristiano katika mechi 54). Muargentina alivunja rekodi  ya Gerd Muller ya mabao 69 ndani ya msimu kwa kufunga mabao 73 msimu  uliopita (ndani ya mechi 60), wakati Mreno Ronaldo alifunga mabao 60  katika mechi 55 msimu uliopita.
Katika  msimu wa sasa,  Messi ameshafunga mabao 57, huku michezo saba ikiwa  imebakia kwenye La Liga, huku kukiwa na uwezekano wa kuwepo kwa michezo  mingine miwili au mitatu kwenye Champions League. Na kama Barca, Madrid  wapo kwenye nusu fainali ya Champions League, hivyo Ronaldo ana karibia  michezo 10 iliyobaki ndani ya msimu kwenye La liga na Champions League,  huku akisubiri fainali ya Copa del Reymwezi ujao, ambapo Real watakutana  na mahasimu wao wa mji mmoja Atletico Madrid katika dimba la Santiago  Bernabeu.
Messi  akiwa na miaka 25, tayari ndio mfungaji bora wa muda wote wa Barcelona  akimpita mkongwe Cesar Rodriguez. Baba Thiago ana mabao 310 katika mechi  375 alizoichezea Barca. Kwa kiwango alichonacho hivi sasa kama  ataendelea kuwa hivi ndani ya misimu mingine minne au mitano anaweza  kufikisha mabao 500 akiwa na jezi ya Blaugrana.
Cristiano,  akiwa na miaka 28, sasa anahitaji mabao manne ili kufikisha mabao 200  akiwa na jezi ya Real Madrid akiendelea kupanda juu kwenye listi ya  wafungaji bora kabisa wa klabu hiyo. 
Anaweza  hata kumpita mchezaji anayeshika nafasi ya tano Hugo Sanchez (Mwenye  mabao 208 ) ndani ya msimu huu, wakati  Alfredo Di Stefano (308) na Raul  (323) anaweza kuwafikia ikiwa ataendelea kuwepo Santiago Bernabeu kwa  miaka miwili mengine.  Akiwa na mabao 196 kwenye  192 games, wastani wa  mabao wa mreno huyo ni mkubwa kuliko wachezaji waliopo kwenye Top 10 ya  wafungaji bora wa Real Madrid. Pia Ronaldo ameshaweka rekodi mpya ya  kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi(11) kwenye ligi ya mabingwa ulaya  ndani ya msimu mmoja.
Messi  ameshasema mara kwa mara kwamba ataendelea kubaki Barcelona kwa miaka  mingi na mashabiki wa Madrid wataendelea kuomba Ronaldo aendelee kubaki  Bernabeu pia. La liga sasa sio tu ni nyumbani kwa vilabu vikubwa na  tajiri zaidi duniani lakini pia ni nyumbani kwa wafungaji bora kabisa  kwenye soka la miaka ya kizazi hiki.
 
 



 
 
 
 
 
 
