Mkongwe wa muziki nchini King Kiki a.k.a Mzee wa Kitambaa cha Cheupe na bendi yake wakitoa burudani kwenye Party ya nguvu iliyoitwa ‘Bongo Balck Ball’ iliyobeba theme ‘Celebrating Tanzanian Music’liliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na masupastaa kibao na wadau wa Tasnia ya Mavazi nchini.
Mbunifu wa Mavazi Khadija Mwanamboka (kulia) ambaye pia ndio mwandaaji wa Party ya Bongo Black Ball iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampuni ya Vitu vya Khadija Events & Clothing inayomilikiwa na mbunifu huyo. Pichani Khadija Mwanamboka na Mbunifu mwenzie Gabriel Mollel wakisakata muziki wa Mzee King Kiki pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
Nainua mkono Mama Kitambaa cheupe…… ishara ya Upendo Mama….. Wageni waalikwa wakiserebuka kwa raha zao ndani ya ukumbi wa Mlimani City.
Wake kwa waume walipeperusha vitambaa vyeupe hewani.
Palinogaje wewe tu ndio umekosekana….
Wageni waalikwa waliendelea kupata burudani kutoka kwa DJ Peter Moe mzee Groove Back kama inavyoonekana pichani.
Wow Amazing…..
Dada Asha Baraka naye alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa.Pichani akijisevia msosi ulioandaliwa maalum kwa wageni waalikwa.
Wageni waalikwa wakiendelea kujipatia dinner ya nguvu maalum kwa ajili yao.
Mdau Khamis wa 361 Degrees naye alikuwepo.
Nyeusi zilitawala ndani ya ukumbi wa Mlimani City.
Wake kwa waume walivunja makabati siku hiyo…Chezea Bongo Black Ball weyeeee!
DJ Peter Moe na DJ Venture wakishow love mbele ya camera yetu.
Ankal Issa Michuzi na Mai waifu wake akishow love na mdau.
Wabunifu wa Mavazi nchini.
Rio Paul na Redd’s Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred wakitoa tabasamu bashasha mbele ya camera yetu.
Kutoka kushoto ni Zainul Mzige, Devotha Diva Mmiliki wa duka la Divas 2006 linapatikana pale maeneo ya Kinondoni Muslim pamoja na Herry Paco Nasser ambaye alipendezesha ukumbi wa Mlimani City na kampuni yake ya Upambaji ya Paco Decor.
Devotha Diva na rafiki yake wakishow love.