Machinga wakiendelea na shughuli zao kama kawaida eneo la mashine Tatu asubuhi hii kutokana na kauli ya mbunge Msigwa kuwaruhusu kurejea ,chini polisi wakiwa eneo hilo
Hali si shwari katika Manispaa ya Iringa baada ya kauli ya mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kuwataka wafanyabiashara wadogop wadogo (machinga) kurejea kufanya kazi katika eneo la barabara ya Mashine tatu kutekelezwa na machinga hao.
Msigwa ambae aliitoa kauli hiyo April 23 mwaka huu katika mkutano wa wabunge wa chadema waliosimamishwa bungeni ,mkutano uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa,kwa kuwataka Machinga kurejea eneo hilo na iwapo mtu atafika kuwanyanyasa basi wana----!!!?
Machinga hao leo wameitikia kauli hiyo kwa kurejea eneo hilo na kupelekea askari wa kutuliza ghasia (FFU) kutanda eneo hilo na kushindwa kutumia nguvu zaidi ya kuwataka wafanyaiashara hao kuendelea na shughuli zao eneo hilo.
Credit francisgodwin
Credit francisgodwin