KLABU ya Manchester United itajaribu kupambana na klabu za Ujerumani, Bayern Munich na Borussia Dortmund kuwania saini ya mshambuliaji wa Dortmund, Robert Lewandowski mwenye thamani ya Pauni Milioni 25.
  Sir Alex Ferguson, ambaye amekuwa  akimfuatilia Lewandowski kwa miezi 18, ana matumaini mapya ya kumnasa  mpachika mabao huyo wa Poland, ambaye alifunga mabao yote manne dhidi ya  Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki hii. 
  United wakati wote inahofia Lewandowski,  ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake atahamia Bayern na  taarifa zinasema amesaini mkataba wa awali wa makubaliano. 

Mshambuliaji wa Borussia Dortmung, Robert Lewandowski (katikati) ni miongoni mwa wachezaji gumzo Ulaya
  Lakini, klabu hizo za Ujerumani zikiwa  katika uwezekano kukutana kwenye Fainali ya Ligi ya Mabingwa Uwanja wa  Wembley baada ya kushinda vizuri mechi za kwanza za Nusu Fainali  nyumbani dhidi ya Barcelona na Madrid, upinzani wao unaweza ukahusika  katika uhamisho wa mchezaji huyu. 
  Tayari mashabiki wa Dortmund wana hasira  za kiungo wao, Mario Gotze kukubali kuhamia Bayern mwishoni mwa msimu  baada ya kufikia makubaliano ya Pauni Milioni 23 na ikiwa Lewandowski  atamfuata mwenzake, inaweza kuwa balaa. 
  Ferguson amepanga Lewandowski akacheze pamoja na Robin van Persie.
  Alisema: "Mashabiki wa Dortmund hawawezi  kufurahia kilichotokea. Sifikiri kama klabu itamuuza Lewandowski kwa  Bayern. Nafikiri wataamua amalizie mkataba wake au wamuuze sehemu  nyingine. 

Anatisha kama njaa: Lewandowski alikuwa kila kitu dhidi ya Real Madrid wiki hii akifunga mabao manne

