Ndege mbili za kampuni ya FastJet zimeondolewa kwenye safari zake na kusababisha usumbufu kwa wateja wanaotumia usafiri huo.
Kampuni hiyo inakabiliwa na hali tete baada ya kudaiwa kuwa wasafiri wake kukosa huduma ya vinywaji na chakula.
Kufutwa kwa safari kulitokea kipindi kifupi baada ya uongozi wa kampuni hiyo kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa wana mpango wa kuongeza safari katika maeneo yenye vivutio vya utalii.
Hivi karibuni, FastJet iliamua kusimamisha huduma ya ndege zake mbili kwa madai ya mvua nyingi zinazoendelea kunyesha nchini.
Kutokana na uamuzi huo, kampuni hiyo imeandika barua kwa mawakala wa kukatisha tiketi kuwaelekeza kurudisha fedha kwa abiria waliokuwa wamewakati tiketi.
Katika taarifa yake kwa mmoja wa wakala wa kukatisha tiketi (jina tunalo) kampuni ya Fastjet inasema kuwa inasikitisha kumjulisha wakala huyo kuwa imebadilisha muda wa safari za ndege yake.
"Tumesimamisha safari kama ifuatavyo. Kilimanjaro kwenda Mwanza kwa ndege namba FN 141/142. Kilimanjaro kwenda Zanzibar kwa ndege namba FN 131/132," ilisema sehemu ya taarifa ya kampuni hiyo.
Taarifa hiyo ilisema safari za ndege hizo zimesimamishwa kuanzia Aprili 18 hadi Juni 30 mwaka huu na kuwa abiria ambao walikwishakata tiketi watarejeshewa fedha zao.
chanzo nipashe