BONDIA Muingereza Amir Khan amedhihirisha  kwamba 'yeye mzima' baada ya kumudu kushinda kwa pointi pambano ambalo  alidondoshwa chini katika raundi ya nne dhidi ya Julio Diaz wa Mexico  jana usiku.
Mpiganaji huyo mwenye umri wa miaka 26,  alikuwa akipigana pambano la pili chini ya kocha mpya, Virgil Hunter  akijaribu kurejesha hadhi yake kwenye ndondi baada ya kupigwa mfululizo  na Lamont Peterson na Danny Garcia.
Khan, mshindi wa Medali ya Fedha katika  Olimpiki ya mwaka 2004 mjini Athens, Ugiriki ushindi wake umetokana na  mafundisho mazuri ya kocha wake mpya, Hunter huko San Francisco. 

Amir Khan akishangilia ushindi wake

Mawindo: Amir Khan akijiandaa kutupa konde

Chini: Diaz akiwa amemuangusha Khan raundi  ya nne, lakini Muingereza huyo aliinuka na kuendelea na pambano hadi  kushinda. Chini anahesabiwa. 


Ua...: Khan akijiandaa kumchapa Diaz

Mpambano ulikuwa mkali...

Kitu cha uhakika: Khan akipiga ngumi ya kutokea chini